JamiiCheck

A citizen-centered approach in countering misinformation and disinformation Online and Offline by JamiiForums

JF Prefixes:

Mdau wa JamiiForums analalamika kuwa alitumia dawa za kutibu Ugonjwa wa Malaria zinazoitwa EKELFIN ambazo baadaye zilimsababishia kupatwa na mchubuko sehemu za siri na midomoni. Anashangaa kwanini Serikali haitoi taarifa kwa watumiaji juu ya madhara ya dawa hizi kwa binadamu. Ni kweli kuwa dawa hizi zinaweza kusababisha athari tajwa?
Katika mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwemo katika jukwaa la JamiiForums.com, kumekuwa na majadiliano na maswali yanahoji au kutoa taarifa ambazo wengi hawana uthibitisho nazo kuhusu dawa za kuzuia maambukizi ya VVU ambazo muhusika anatakiwa kutumia ndani ya masaa 72. Je, hili lina ukweli? Na inakuaje kwa muhitaji ambaye si muhanga, na gharama zake zikoje? Je, kuna ukweli kwenye hili?
Kuna wazandiki huwa nawashangaa wanavyoponda pombe. Pombe haina madhara kama wanafiki wanavyotuaminisha. Pombe ni nzuri ukinywa kistaarabu, ina faida lukuki, ukibisha muulize Albert Chalamila. Tafiti zinasema kuwa beer zinasaidia kujilinda na magonjwa ya moyo. Kama mnavyojua magonjwa ya moyo yanaondoa watu kimya kimya hivyo mimi nawashauri tunywe beer kujilinda na magonjwa ya moyo. Hata Biblia inasisitiza tunywe pombe tufurahie, na mkituona tunakunywa pombe msitukwaze. Too much of anything is bad, but too much good whiskey is barely enough
Leo nimeona video ambao imewekewa sauti ya mtu akisema wametumiwa video hiyo kwenye group la shule ya Themihill, video hiyo inaonesha mtu akifungua kitu kinachoonekana kama pen (kalamu) ambacho ndani yake kina risasi na baadaye kufyatuliwa. Anayeelezea video hiyo anadai pen hizo zinagawiwa mashuleni na kuuzwa huku akionesha hofu ya watoto kuuana au wao wenyewe kujidhuru kwa peni hizo. Ningependa kufahamu ukweli kuhusu video hiyo.
Kumekuwepo na madai yanayosambaa mtandaoni kuwa makasha ya dawa za meno huwa na rangi (code) za aina mbalimbali zinazofafanua aina ya kemikali zilizotumika kutengenezea dawa hiyo. Aidha, madai hayo yanafafanua zaidi kuwa kemikali husika ni hatari kwa afya na husababisha saratani, na kwamba makampuni yanayozalisha dawa hizi hayawezi kukupa siri hii. Ukweli wake upoje?
Habari, Ninanukuu kutoka kwenye meseji iiyotummwa kwenye kundi moja la Telegram ambalo mimi pia nimo. Huku mitaani kuna taarifa kuwa kuwa uvunaji wa damu unaifanyika maeneo mbalimbali nchi huwa siku hizi hawatupi damu yoyote hata kama wataikuta ina ugonjwa wowote kwa kuwa damu hiyo wata muongezea mtu mwenye ugonjwa ulipo kwenye damu, mfano wakakuta damu waliyovuna ina virusi vya ukimwi hawaitupi akija mgonjwa mwenye ukimwi basi wata muongezea damu hiyo je hii ni kweli? Inasadikika hili limechangiwa na ugumu wa kupata damu lakini pia hakuna shida yoyote mfano mtu ana virusi vya UKIMWI akiongezewa damu ya virusi vya UKIMWI kwa kuwa tatizo lake hapo ni damu si salama au isiyo salama, eti hata kama wangemuongezea damu iliyo salama bado...
Wakuu, Nimekuja na swali hili baada ya jamaa mmoja kusema jambo hili sio la kweli, lakini mimi pia nimeshawahi sikia hii, bi mkubwa alituhadisia kuna ndugu yao mmoja aling'atwa na mbwa mwishowe alipokaribia kwenda kwenye ulimwengu mwingine alikuwa akibweka kama mbwa. Naamini hata wewe unayesoma hapa umeshawahi kusikia kuhusu hili. Je, suala hili ni kweli au stori tu za mtaani wataalamu wa JamiiCheck?
Alhamisi ya pili ya Mwezi Machi kila mwaka, Dunia huadhimisha Siku ya Figo Duniani ili kutoa ufahamu na kuelimisha umma kuhusu umuhimu wa afya ya figo na magonjwa yanayohusiana na figo. Kupitia maadhimisho haya, watu hupata fursa ya kujifunza kuhusu njia za kuzuia magonjwa ya figo, kudhibiti magonjwa ya figo, na umuhimu wa kuwa na maisha yenye afya ya figo. Aidha, maadhimisho haya huchangia katika kuongeza uelewa wa umma kuhusu haja ya kuchangia katika juhudi za kuzuia na kutibu magonjwa ya figo, pamoja na kusaidia watu wenye matatizo ya figo kupata msaada unaohitajika. Hata hivyo, ugonjwa huu huambatana na dhana nyingi potofu zinazofifisha kasi ya kupambana nao hivyo JamiiCheck imekuandalia ufafanuzi wa Dhana hizo kama sehemu ya...
Back
Top Bottom